Matembezi ya kuchangisha fedha mkoa wa Kagera yameongozwa na Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi mjini DSM na kuchangisha zaidi ya Shs.Milioni mia tano. Prof Anna Tibaijuka Mbunge wa Muleba Kusini na pia Mwenyekiti wa waBunge Mkoa wa Kagera alishiriki na kutoa neno la shukrani baada ya Mbunge wa Bukoba Manispaa Mhe Wilfred Lwakatare kuelezea […]
Manama, Aug. 30 (BNA): His Royal Highness Prime Minister Prince Khalifa bin Salman Al Khalifa has approved the nomination of Professor Anna Tibaijuka, former Minister of Lands, Housing and Human Settlement Developments in Tanzania, former Under-Secretary-General of the United Nations and Executive Director of the United Nations Human Settlements Programme (UN-HABITAT), to win the “His […]
MULEBA 15 JULAI 2016 Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametembelea Wilaya ya Muleba na kufika Rubya, hospitali teule ya Wilaya inayomilikiwa na kanisa katoliki. Alipokelewa kwa shangwe kubwa na wafanyakazi na wauguzi wanafunzi wote wakiongozwa na Mwashamu Askofu Methodius Kilaini, Mkuu wa Wilaya ya Muleba, mkuu wa Mkoa, na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini […]
Tarehe 15-03-2016 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa atoa pole kwa Mbunge wa Muleba Kusini,Profesa Anna Tibaijuka kwa kufiwa na mama yake mzazi Ma Aurelia Kajumulo.Waziri mkuu aliongozana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dk. Medard Kalemani na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni . Share on:
Share on:
Tarehe 05-02-2016 Mh Prof Anna Tibaiujuka,mbunge wa Muleba Kusini ameshiriki katika kikao cha Halmashauri ya wilaya ya Muleba kilichofanyika wilayani Muleba Share on:
Mbunge wa Muleba Kusini Prof Anna Tibaijuka, ameshiriki mazishi ya aliyekuwa diwani kata ya Kimwani Marehemu Faustine Muliga (CUF) aliyeuawa kwa kushambuliwa kwa mapanga na watu wasiojulikana. Share on:
Tarehe 8-01-2016 Hayati Balozi Wilson Tibaijuka,mume wa Prof Anna Tibaijuka angefikisha miaka 71 ya kuzaliwa.Pichani ni mwaka 1988 akiwa amembeba mwanae Kagem nyumbani kwao Makongo juu jijini Dar es salaam.Balozi Tibaijuka alifariki mwaka 2000 akiwa na umri wa miaka 55.Apumzike kwa amani Share on:
Mbunge wa Muleba Kusini Mh. Prof Anna Tibaijuka ,ameshiriki katika ufunguzi wa mkutano wa maendeleo ya manispaa ya Bukoba,Bukoba Municipal Developmental Conference(BUMUDECO) uliyofanyika tarehe 27-12-2015 mjini Bukoba.Walioudhulia mkutano huo ni pamoja na mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Mh.Wilfred Lwakatare,Bw. James Rugemalila,Askofu Methodius Kilaini pamoja na wadau wengineo wa maendeleo(Picha na Mansoor Amri Kahauza) Share on:
Mbunge wa Muleba Kusini Mh. Prof Anna Tibaijuka ameshiriki misa katika kanisa la Kasaidolo mjini Bukoba jumapili ya tarehe 27/12/2015.Baada ya misa mheshimiwa alishiriki katika kikao kilichofanyika kanisani hapo.(Picha na Mansoor Amri Kahauza) Mh. Anna Tibaijuka katika picha ya pamoja na Askofu Methodius Kilaini, Kulia ni Mama Rugimbana. Share on:
Share on:
15-12-2015 Mbunge wa Muleba Kusini Prof Anna Tibaijuka ameshinda kesi ya malalamiko ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Muleba Kusini ndugu Kashasla.Jaji wa mahakama kuu mkoa wa Kagera ameondoa shataka hilo.(Picha na Mansoor Amri Kahauza) Share on:
09/12/2015 Prof Anna Tibaijuka,Mbunge wa Muleba Kusini akiadhimisha sikukuu ya Uhuru(miaka 54 ya uhuru) kwa kufanya usafi wa mazingira pamoja na wakazi wa Muleba Kusini katika kutekeleza agizo la Raisi John Pombe Magufuli. (Picha na Mansoor Amri Kahauza) Share on:
Mbunge wa Muleba Kusini, Prof Anna Tibaijuka akiwa katika kikao cha baraza la Madiwani mara baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba ambapo Bw. Kamugisha aliibuka mshindi kwa akupata kura 45.(Picha na Mansoor Amri Kahauza) Share on:
Tarehe 6/12/2015 Mbunge wa Muleba Kusini,Prof Anna Tibaijuka audhuria kikao cha kumchagua mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya aya Muleba ambapo ndugu Kamugisha diwani kata ya Kikuku alipata kura 34 na ndugu Magongo diwani kata ya Muhutwe alipata kura 10. Share on: