Prof  Anna Kajumulo Tibaijuka

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametembelea Wilaya ya Muleba na kufika Rubya, hospitali teule ya Wilaya inayomilikiwa na kanisa katoliki.

MULEBA 15 JULAI 2016

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametembelea Wilaya ya Muleba na kufika Rubya,  hospitali teule ya Wilaya inayomilikiwa na kanisa katoliki. Alipokelewa kwa shangwe kubwa na wafanyakazi na wauguzi  wanafunzi wote wakiongozwa na Mwashamu Askofu Methodius Kilaini,  Mkuu wa Wilaya ya Muleba, mkuu wa Mkoa, na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Prof Anna Tibaijuka.

Waziri alifanya kikao na wafanyakazi wa hospitali na kuwahakikishia kuwa serikali itaendelea kushirikiana na hospitali za misheni kutoa huduma. Aidha waziri alisema hospitali ya Rubya ina sifa kubwa na kuwapongeza kwani ameelezwa hakuna  tatizo la wafanyakazi hewa. Waziri alitembelea wodi ya akina mama waliojifungua na kupongeza viwango vya usafi na huduma.

Waziri alishauri kuwa haoni sababu ya kujenga hospitali nyingine kwa sasa na kipaumbele kiwe ni kuimarisha hospitali ya Rubya na huduma za upasuaji katika vituo vya Afya Kaigara na Kimeya. Waziri alihimiza uhamasishaji wa watu kujiunga na bima ya afya na kusema sasa kwa Shs 30, 000/- mtu atibiwe hosptali ya Rufaa ya mkoa.

Akimshukuru kwa uchapaji kazi makini na kuwatembelea mapema baada ya kupewa kazi ya Uwaziri wa Afya Mbunge wa Muleba Kusini Profesa Tibaijuka alisema Wilaya ina wakazi karibu lhaki moja visiwani ambao hawana huduma za afya zenye uhakika. Bajeti inayotolewa izingatie mazingira ya Wilaya ambayo ni magumu.  Mbunge alisema tunahitaji boats kwenda visiwani siyo magari. Pia Mbunge alisema wilaya ni kubwa ina kata 43 na hivyo inahitaji Vituo vya afya vingi zaidi. Profesa pia aliomba ambulance nyingine maana iliyopo ilitolewa na  Waziri wa afya wa zamani Hussein Mwinyi na haitishi. Mbunge alikuvali mwito wa waziri wa kutoa hamasa kwa wananchi kujiunga na bima ya afya lakini akaomba bima hiyo kwa mkoa wa Kagera iwawezeshe wagonjwa kupewa huduma hospitali ya Bugando Mwanza kwani ndiyo hutumika kuwapeleka wagonjwa wanaozidiwa.

Waziri alifuatana na Bi Janean Davis Mkuu wa Miradi ya Afya ofisi za USAID na dr Dunstan Bishanga Mkuu wa mradi wa Mama na Mtoto JHPIEGO kutoka dar es salaam.

Wageni wengine walitoka ofisi za Congressman John Payne wa New Jersey Marekani ambaye alifanya kazi kwa karibu na Profesa Anna Tibaijuka alipokuwa bado Umoja wa Mataifa. Wageni hao wamefurahia sana kumkuta Profesa nyumbani. Wamefurahia mazingira  ya Rubya na kuahidi kutafuta misaada zaidi.

Posted by on Jul 16 2016. Filed under Muleba South Constituency, Prof Tibaijuka's Daily Photo News. You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Both comments and pings are currently closed.

Comments are closed

Photo Gallery

Log in | This website is Designed & Maintained by Noel Mubeya