24/02/2017 Prof Anna Tibaijuka audhulia mdahalo wa wanafunzi wa Barbro Johansson na Shule ya sekondari ya Pugu
Mdahalo wa wanafunzi wa Barbro School ya DSM na wageni wao kutoka Shule ya Wavulana ya Pugu. Profesa amekaa na Mwl Mkuu Halima Kamote na wanafunzi kutoka Sweden ambao wanatembelea shule hiyo.
Mada Ilikuwa “Ugunduzi wa Sayansi na Technologia umeweka maisha ya mwanadamu hatarini”.
Barbro ilikuwa inatetea mada ikiwa upande wa Serikalu na Pugu Boys walikuwa wanapinga mada wakiwa upande wa upinzani.
Walitumia mgumo wa Bunge la Uingereza wa Waziri Mkuu na mawaziri wake na kiongozi wa upinzani na mawaziri wake vivuli.
Mdahalo ulikuwa wa kusisimua sana. Mtetea hoja aliorodhesha matatizo kadhaa yaliyosababishwa na ugunduzi wa sayansi na teknologia ikiwemo upweke maana sasa kila mtu anaongea na simu yake badala ya jirani yake; vita kama vya nuklea vilivyoimaliza Hiroshima na Nagasaki kwa mzinga wa atomic. Ukatili na kutojali jamii kwa sababu ya kuiga tabia hizo kutoka action movies; magonjwa kibao ikiwemo ya vidole yanayosababishwa na mionzi ya simu za mkononi; kukua kwa saratani na watu kukosa ajira kwa sababu machine zimechukua kazi hizo. Pia uchafuzi wa mazingira.
Akipangua hoja Waziri Mkuu kivuli wa Pugu alisema bila sayansi na teknologia hakuna elimu hakuna mawasiliano hakuna maendeleo hakuna ulinzi na usalama. Viwanda ambavyo Rais anasisitiza vinahitaji sayansi na teknologia.
Ukumbi ulukuwa wa furaha sana. Waamuzi wawili mmoja kutoka kila upande waliona mshindi ni Barbro kwa sababu walijitahidi sana kujenga hoja.
Akiongea na wanafunzi hao baada ya mdahalo Profesa aliwapongeza ila kuwahimiza wanafunzi wa kike waliokuwa wenyeji kutokuwa na aibu na kuchukua majukumu ya kiuongozi. Alisema alishangaa kuona kwamba pamoja na kuwa Pugu Boys ndio walikuwa wageni waliobekana kuongoza shughuli nzima huku wenyeji wakibaki kuelekezwa. Aliwakosoa pande zote katika hilo na kusema shule ya Barbro inamtayarisha msichana kujisimamia katika kutekeleza wajibu wake. Kwa hiyo siku nyingine mgeni achukue nafasi yake ya kuelekezwa na kukaribishwa na mwenyeji.
Tukio hili limeonyesha jinsi shule za viwango zinavyotoa elimu nje ya vitabu na kujenga uwezo na uzoefu wa wanafunzi.
Taarifa ya Frank Emmanuel