Prof  Anna Kajumulo Tibaijuka

Mtandao wa Equality For Her umemtaja Prof.Tibaijuka miongoni mwa wanawake majasiri,hodari shujaa ktk kupigania haki za wanawake na maendeleo kwa ujumla Duniani.

Mtandao wa Equality For Her umemtaja Prof.Tibaijuka miongoni mwa wanawake majasiri,hodari shujaa ktk kupigania haki za wanawake na maendeleo kwa ujumla Duniani.Mtandao huu wenye makao yake makuu New York nchini Marekani,ni mtandao ambao umekua ukitambua na kuenzi juhudi na mchango wa wanawake hodari na jasiri duniani kote katika kupigania haki na maendeleo.Kwa mara ya kwanza Mtanzania pekee amepata bahati ya kutajwa katika mtandao huo kwa kutambua mchango wake katika nyanja tofauti za kimaendeleo Duniani na katika kuendesha harakati za wanawake.Itakumbukwa kuwa Tibaijuka mbali na kushika nyadhifa mbali mbali duniani,lakini pia ni mwanaharakati wa kutetea  haki na maendeleo ya wanawake,anatambuliwa kwa kuanzisha BALAZA LA WANAWAKE TANZANIA (BAWATA),ambapo yeye ndiye mwenyekiti wake, ni mwanzirishi wa taasisi ya JOHA TRUST ambayo inasimamia na kuendesha shule bora za mfano kwa wasichana hapa nchini,Akiwa umoja wa mataifa alianzisha taasisi mbalimbali za kutetea haki na usawa wa wanawake kumiliki ardhi hasa kwa bara la Afrika,badhi yake ni UGWLAT-UGANDA,KEWLAT-KENYA,TAWLAT-TANZANIA,ZIWLAT-ZIMBABWE…. na sehem zingine nyingi Afrika.Haya ni baadhi ya mambo ambayo yanasababisha mwanamke huyu kuendelea kutambuliwa sehemu mbalimbali duniani katika kuchangia maendeleo.Miongoni mwa wanawake wengine walio tajwa na mtandao huo ni walio wahi kushika nyadhifa za uraisi na kuleta mapinduzi katika nchi zao,wanaharakati mbali mbali Duniani kama Kamala Harris,mmarekani mweusi wa kwanza kuwa mwanasheria mkuu Calfornia,Ursula Burns CEO  na mwenyekiti wakwanza mwanamke kuongoza zaidi ya kampuni 500 za Fortune.Wengine ni Shirley Chisholm,Tasneem Zehra Husain,Yu Su-May na wengine wengi.Heko kwa Prof.Tibaijuka????

Posted by on Mar 11 2017. Filed under Prof Tibaijuka's Daily Photo News. You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Both comments and pings are currently closed.

Comments are closed

Photo Gallery

Log in | This website is Designed & Maintained by Noel Mubeya