10-02-2016 Mapokezi ya ambulance hospitali ya wilaya Rubya Jimbo la Muleba Kusini kama utekelezaji wa ahadi husika
Hatimaye yaliyotabiriwa sasa yametimia. Mtakumbuka kuwa mnamo tarehe 19. 09.2016 Wakati wa Ziara ya Mh. Waziri Ummy Mwlm. Muleba kule Rubya Hospital.
Mh. Mbunge Prof. Tibaijuka alimuomba Mh. Waziri kuwa baada ya Kaigara na Kimeya kupata Ambulance, ni vema tukapata Ambulance nyingine hapa Hospitali teule ya Rubya.
Mh. Waziri alikubali na leo hatimaye ahadi imetimia. Leo hii Uongozi wa Rubya umepokea rasmi Ambulance husika kama utekelezaji wa ahadi husika
Tunachukua nafasi hii kuwapongeza Wana Muleba kwa kupata Ambulance husika. Shukran zimwendee mtoa maombi na mfuatiliaji Mh. Prof. Tibaijuka a.k.a Akalandalugo kuhakikisha sasa Muleba tutakuwa na Ambulance 4, kwa maana kwamba Rubya, Kimeya na Kaigara. Ile nyingine ipo Kishuro kwa Mh. Mwijage Jimbo la Muleba Kaskazini.
Naambatanisha picha za makabidhiano.