Prof  Anna Kajumulo Tibaijuka

Matembezi ya kuchangisha fedha mkoa wa Kagera yameongozwa na Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi mjini DSM 17-09-2016

WhatsApp Image 2016-09-17 at 15.13.09Matembezi ya kuchangisha fedha mkoa wa Kagera yameongozwa na Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi mjini DSM na kuchangisha zaidi ya Shs.Milioni mia tano.

Prof Anna Tibaijuka Mbunge wa Muleba Kusini na pia Mwenyekiti wa waBunge Mkoa wa Kagera alishiriki na kutoa neno la shukrani baada ya Mbunge wa Bukoba Manispaa Mhe Wilfred Lwakatare kuelezea matatizo yaliyokumba Mkoa wa Kagera. Matembezi yaliandaliwa na Wizara ya Mambo ya nchi za nje na kuhudhuriwa na mamia ya watu wakiwemo mabalozi kutoka nchi za nje wafanya biashara na viongozi wengine wakuu wa serikali wakiwemo mawaziri makatibu wakuu na mashirika ya umma makampuni binafsi na taasisi za kidini na kijamii.

Pichani Rais Mwinyi akiongoza matembezi akiwa na mwenyeji wake Mhe Balozi Augustine Maige Waziri wa Mambo ya Nje, Katibu Mkuu kiongozi Mhe Balozi John Kijazi na Mhe Prof Tibaijuka (Mb) kwa niaba ya watu wa Kagera.
WhatsApp Image 2016-09-17 at 11.54.24 WhatsApp Image 2016-09-17 at 15.09.28 WhatsApp Image 2016-09-17 at 15.13.09 WhatsApp Image 2016-09-17 at 15.24.25 WhatsApp Image 2016-09-17 at 15.50.31

Posted by on Sep 17 2016. Filed under Muleba South Constituency, Prof Tibaijuka's Daily Photo News. You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Both comments and pings are currently closed.

Comments are closed

Photo Gallery

Log in | This website is Designed & Maintained by Noel Mubeya