Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atoa pole kwa Prof. Anna Tibaijuka kwa kufiwa na mama yake
Tarehe 15-03-2016 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa atoa pole kwa Mbunge wa Muleba Kusini,Profesa Anna Tibaijuka kwa kufiwa na mama yake mzazi Ma Aurelia Kajumulo.Waziri mkuu aliongozana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dk. Medard Kalemani na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni .

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa(kulia),akimpa pole Mbunge wa Muleba Kusini,Profesa Anna Tibaijuka,ambaye amefiwa na mama yake

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa,akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa mama wa Mbunge wa Muleba Kusini,Profesa Anna Tibaijuka, alipofika kutoa pole kwa wafiwa Muleba.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(kulia),akimpa pole Mbunge wa Muleba Kusini,Profesa Anna Tibaijuka, aliyefiwa na mama yake,marehemu Ma Aurelia Kajumulo.















