
Tarehe 15-03-2016 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa atoa pole kwa Mbunge wa Muleba Kusini,Profesa Anna Tibaijuka kwa kufiwa na mama yake mzazi Ma Aurelia Kajumulo.Waziri mkuu aliongozana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dk. Medard Kalemani na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni . Share on:

Mhe, Prof. Anna Tibaijuka mbunge wa muleba kusini anasikitika kutangaza kifo cha Mama yake mzazi Ma Auleria Kajumulo kilichotokea leo alhamisi tarehe 10.3.2016 katika hospitali ya kagondo msiba upo nyumbani kwa Profesa kagabilo tarehe ya mazishi itatangazwa baadae wanasubiliwa ndg kutoka Ulaya na Marekani. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe Amina. Share on:

Tarehe 05-02-2016 Mh Prof Anna Tibaiujuka,mbunge wa Muleba Kusini ameshiriki katika kikao cha Halmashauri ya wilaya ya Muleba kilichofanyika wilayani Muleba Share on:

Mbunge wa Muleba Kusini Prof Anna Tibaijuka, ameshiriki mazishi ya aliyekuwa diwani kata ya Kimwani Marehemu Faustine Muliga (CUF) aliyeuawa kwa kushambuliwa kwa mapanga na watu wasiojulikana. Share on:

Muanzilishi wa Baraza la Wanawake Tanzania(BAWATA) Prof Anna Tibaijuka (mb) amekutana na waasisi wa BAWATA Kinondoni Dar es salaam tarehe 11-01-2015. Share on:

Tarehe 8-01-2016 Hayati Balozi Wilson Tibaijuka,mume wa Prof Anna Tibaijuka angefikisha miaka 71 ya kuzaliwa.Pichani ni mwaka 1988 akiwa amembeba mwanae Kagem nyumbani kwao Makongo juu jijini Dar es salaam.Balozi Tibaijuka alifariki mwaka 2000 akiwa na umri wa miaka 55.Apumzike kwa amani Share on:

Mbunge wa Muleba Kusini kwa tiketi ya CCM Mh. Prof Anna Tibaijuka amekutana na balozi wa Sweeden nchini Tanzania tarehe 7-1-2016 jijini Dar es salaam. Share on:

Mbunge wa Muleba Kusini Mh. Prof Anna Tibaijuka ,ameshiriki katika ufunguzi wa mkutano wa maendeleo ya manispaa ya Bukoba,Bukoba Municipal Developmental Conference(BUMUDECO) uliyofanyika tarehe 27-12-2015 mjini Bukoba.Walioudhulia mkutano huo ni pamoja na mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Mh.Wilfred Lwakatare,Bw. James Rugemalila,Askofu Methodius Kilaini pamoja na wadau wengineo wa maendeleo(Picha na Mansoor Amri Kahauza) Share on: