Prof  Anna Kajumulo Tibaijuka
Archive for: December, 2015

Prof Anna Tibaijuka,mbunge wa Muleba Kusini ashiriki katika mkutano wa Maendeleo ya Manispaa ya Bukoba(BUMUDECO)

Mbunge wa Muleba Kusini Mh. Prof Anna Tibaijuka ,ameshiriki katika ufunguzi wa mkutano wa maendeleo ya manispaa ya Bukoba,Bukoba Municipal Developmental Conference(BUMUDECO) uliyofanyika tarehe 27-12-2015 mjini Bukoba.Walioudhulia mkutano huo ni pamoja na mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Mh.Wilfred Lwakatare,Bw. James Rugemalila,Askofu Methodius Kilaini pamoja na wadau wengineo wa maendeleo(Picha na Mansoor Amri Kahauza) Share on:

Jumapili ya 27/12/2015 Prof Anna Tibaijuka(MB) ashiriki misa kanisa la Kasaidolo,mjini Bukoba

Mbunge wa Muleba Kusini Mh. Prof Anna Tibaijuka ameshiriki misa katika kanisa la Kasaidolo mjini Bukoba jumapili ya tarehe 27/12/2015.Baada ya misa mheshimiwa alishiriki katika kikao kilichofanyika kanisani hapo.(Picha na Mansoor Amri Kahauza) Mh. Anna Tibaijuka katika picha ya pamoja na Askofu Methodius Kilaini, Kulia ni Mama Rugimbana.   Share on:

19-12-2015 Mbunge wa Muleba Kusini,Prof Anna Tibaijuka atembelea mnada wa Mbunda uliyopo Muleba

Share on:

Prof Anna Tibaijuka(MB) ameshinda kesi ya malalamiko ya uchaguzi iliyofunguliwa dhidi yake

15-12-2015 Mbunge wa Muleba Kusini Prof Anna Tibaijuka ameshinda kesi ya malalamiko ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Muleba Kusini ndugu Kashasla.Jaji wa mahakama kuu mkoa wa Kagera ameondoa shataka hilo.(Picha na Mansoor Amri Kahauza) Share on:

Prof Anna Tibaijuka,Mbunge wa Muleba Kusini akishiriki zoezi la usafi pamoja na wakazi wa Muleba Kusini

09/12/2015 Prof Anna Tibaijuka,Mbunge wa Muleba Kusini akiadhimisha sikukuu ya Uhuru(miaka 54 ya uhuru) kwa kufanya usafi wa mazingira pamoja na wakazi wa Muleba Kusini katika kutekeleza agizo la Raisi John Pombe Magufuli. (Picha na Mansoor Amri Kahauza) Share on:

Prof Anna Tibaijuka akiwa katika kikao cha baraza la Madiwani

Mbunge wa Muleba Kusini, Prof Anna Tibaijuka akiwa katika kikao cha baraza la Madiwani mara baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba ambapo Bw. Kamugisha aliibuka mshindi kwa akupata kura 45.(Picha na Mansoor Amri Kahauza)   Share on:

Prof Anna Tibaijuka audhuria kikao cha kumchagua mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba

Tarehe 6/12/2015 Mbunge wa Muleba Kusini,Prof Anna Tibaijuka audhuria kikao cha kumchagua mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya aya Muleba ambapo ndugu Kamugisha diwani kata ya Kikuku alipata kura 34 na ndugu Magongo diwani kata ya Muhutwe alipata kura 10. Share on:

Photo Gallery

Log in | This website is Designed & Maintained by Noel Mubeya