Prof  Anna Kajumulo Tibaijuka

Ziara ya Prof Anna Tibaijuka(MP) jimboni Muleba Kusini

19826_807095832717160_2827531526124747705_n

Kutokana na ubovu wa barabara Prof Tibaijuka alilazimika kuacha gari lake Kyota na kupanda pikipiki kwa umbali wa kilometa 13 na hatimaye alishuka na kutembea kwa miguu umbali wa kilometa 2 ambapo alitelemka mlima mkali hadi Kaazi Nyakishabo

Mbunge wa muleba kusini Prof  Anna Tibaijuka alitembelea kata ya kimwani kijiji cha kaguramo kitongoji cha kaazi nyakishabo na kulakiwa namamia ya wananchi waliopanda mlimani wakiwa na matawi ya miti huku wakiimba. Kaazi ni kambi kubwa ya wavuvi

Mwenyekiti wa kitongoji cha Kaazi Nyakishabo Ndugu Ojax Dorolyma Lyapa alionyesha furaha yake kwa kusoma risala ya kijiji kwa lugha ya kimombo huku akishangiliwa alipokuwa anaitafsiri. Mwenyekiti huyo alisema ProfTibaijuka ametengeneza historia kuwa Mbunge wa kwanza tangu uhuru kufika kwenye kijiji hicho kilicho mwambao wa ziwa.

Pro Tibaijuka aliwasili Kyota majira ya saa 11 jioni akiwa amechelewa akitokea Bukoba ambapo alilazimika kuhudhuria kikao cha kamati ya siasa ya mkoa ya chama cha mapinduzi ambamo yeye ni mjumbe.

Kwa ubovu wa barabara Prof aliacha gari yake Kyota na kupanda pikipiki kilometa 13 hadi kaguramo mwisho ambapo alishuka na kutembea kilometa 2 kutelemka mlima mkali hadi Kaazi Nyakishabo.

Kutokana na ubovu wa barabara Prof Tibaijuka alilazimika kuacha gari lake Kyota na kupanda pikipiki kwa umbali wa kilometa 13 na hatimaye alishuka na kutembea kwa miguu umbali wa kilometa 2 ambapo alitelemka mlima mkali hadi Kaazi Nyakishabo

Kutokana na ubovu wa barabara Prof Tibaijuka alilazimika kuacha gari lake Kyota na kupanda pikipiki kwa umbali wa kilometa 13 na hatimaye alishuka na kutembea kwa miguu umbali wa kilometa 2 ambapo alitelemka mlima mkali hadi Kaazi Nyakishabo

Alishuhudia mamia ya watoto wa shule ya msingi wanaolazimika kutembea kilometa 7 kila siku kwenda shule ya msingi kaguramo.
Mwenyekiti wa kijiji aliomba prof tibaijuka akubali kufadhili ujenzi wa shule ya msingi itakayojulikana kwa jina lake kijijini hapo. Bila kumungunya maneno mwenyekiti huyo wa ccm alimtaka prof kuendelea na ubunge wa jimbo hilo kuleta maendeleo.

Prof alianza hotuba yake kwa kuwataka watoto wasiokwenda shule kijitokeza. Mtoto
Abdu akaja mbele na kusema ameacha darasa la 3 kwa kukosa sare ya shule. Papo kwa papo prof tibaijuka alitoa fedha za kumshonea sare. Prof pia akachanga lhakib 2 na nusu mfuko kuwasaidia watoto wahitaji waendelee na masomo. Prof akaafiki kushirikiana na wanakijiji kujenga shule ya msingi baada ya kuambiwa kijiji cha nyakishabo kina kaya 400. Prof alisema atawasiliana na Halmashauri kuhusu suala hilo.

Mwenyekiti wa kijiji aliorodhesha kero ya umeme barabara na prof akaafiki na kuahidi kuzifanyia kazi. Prof alitoa michango mbalimbali kwa vikundi vya wanawake na vijana waliosoma risala zao jumla milioni mbili na nusu.

Mkutano wa Kyota uliahirishwa kwa usiku kuingia hata hivyo prof aliwasalimia wananchi wsliomdubiri hadi usiku na kuahidi kurejea siku nyingine.

11083676_807097499383660_1088182288880559125_n

 

IMG_5816

IMG_5851

IMG_5873

IMG_5886

IMG_5905

Posted by on Mar 24 2015. Filed under Daily Photo, Muleba South Constituency. You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Both comments and pings are currently closed.

Comments are closed

Photo Gallery

Log in | This website is Designed & Maintained by Noel Mubeya