Tarehe 21/11/2016 Prof.Tibaijuka ameshiriki mkutano wa Wiki ya Maji Kenya uliofanyika katika ukumbi wa Kenyatta International Conference Centre(K.I.C.C)
Tarehe 21/11/2016 Prof.Tibaijuka ameshiriki mkutano wa Wiki ya Maji Kenya. Mkutano umefanyika katika ukumbi wa KENYATTA INTERNATIONAL CONFERENCE CENTRE (K.I.C.C) na kushirikisha wadau na taasisi mbalimbali duniani. Miongoni mwa washiriki ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji Kenya Mhe.Eugene Wamalwa, naibu Waziri mkuu na Waziri wa mambo ya nje wa Ubelgiji Mhe. Didier Reynders. Pamoja na viongozi wakuu wa nchi ya Kenya, wakuu wa taasisi mbalimbali na mabalozi. Prof. Tibaijuka anamwakilisha Dr . Chris Williams ambaye ndie mkurugenzi wa shirika la WSSCC.Katika mkutano huo Prof.Tibaijuka anahimiza sana umuhimu wa Maji, kutunza vyanzo vya Maji na mazingira. Anahimiza pia umuhimu wa usafi kwani mambo haya yanaenda kwa pamoja. Katika mkutano huo prof. Tibaijuka alikuwa kivutio kwa mada zake moto moto na ujumbe wake. Amehimiza serikali zote kutasahau wala kuacha nyuma suala la usafi. Jambo hili lilipelekea Waziri wa Maji kubadili Jina la mkutano na kukubali pendekezo la prof.Tibaijuka kwamba kuanzia mwakani mkutano hautaitwa tena Kenya Water Week, badala yake utaitwa Kenya Water Week and Sanitation ili kutosahau kuhimiza juu ya usafi kama alivyo pendekeza prof.Tibaijuka