Prof  Anna Kajumulo Tibaijuka

Maombi ya dharura kutoka kwa mbunge wa Muleba Kusini kwenda kwa RC Mwanza kufuatia uvamizi wa majambazi katika kisiwa cha CHAKAZIMBWE kata ya Ikuza

RC Mwanza.
Mkuu. Nakuletea maombi ya dharura. Tarehe 04/04/2016 kisiwa CHAKAZIMBWE KATA IKUZA WILAYA MULEBA majambazi yenye silaha yalivamia na kuiba injini 13 na mtumbwi 1. Halafu yakakimbilia WILAYA YA UKEREWE KISIWA GANA. Mapolisi kutoka Mazinga Muleba na wavuvi wakiongozwa na Afande James (0757940273 ) na Hamis(0784894837) wamefuatilia huko GANA siku 3 sasa. Wamefanikiwa kukamata mashine 1. Kwa mujibu wa taarifa ya Diwani wa Mazinga Mhe Alex (0682627888) mapolisi waliotoka mazinga muleba wamekosa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wenyeji wao huko GANA UKEREWE. Inadaiwa mapolisi wa GANA UKEREWE wanashirikiana na majambazi hao. Naomba uchunguze na kutusaidia ipasavyo. Nakala DC MULEBA OCD MULEBA RC KAGERA. Nawasilisha na nitashukuru mrejesho niwatulize wananchi. Ujambazi ziwa victoria ni kero ambayo Mhe Rais wetu aliahidi kutokomeza. Tusimuangushe.

Mama Tibaijuka Mbunge Muleba Kusini

Posted by on Apr 10 2016. Filed under Prof Tibaijuka's Daily Photo News. You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Both comments and pings are currently closed.

Comments are closed

Photo Gallery

Log in | This website is Designed & Maintained by Noel Mubeya