Prof  Anna Kajumulo Tibaijuka

Profesa Anna Tibaijuka amehudhuria mazishi ya Mama Peras Wilhelmina Ngombale Mwiru yaliyofanyika jijini Dar es Salaam

Pamoja na changamoto ya kuuguza mdogo wake Richard hapo Muhimbili Mbunge wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka amehudhuria mazishi ya Mama Peras Wilhelmina Ngombale Mwiru yaliyofanyika jijini Dar es Salaam katika kanisa la St Peters halafu makaburi ya Kinondoni.

Picha zinaonyesha umati wa watu na viongozi wa chama na serikali waliokusanyika kuungana na familia ya Mzee Kingunge kumuaga mkewe. Marehemu Mama Ngombale alifariki tarehe 4/01/2018 katika hospitali ya muhimbili kwa matatizo ya kisukari. Mama Ngombale alikuwa Mzaliwa wa kijiji cha Ilogero Kamachumu Wilaya ya Muleba. Wasifu wake umeonyesha mke wa kiongozi mahili aliyekuwa anafanya kazi za chama na serikali bila kujitangaza. Ni mwanzilishi wa vituo vya kulea watoto yatima SOS villages na pia Mwenyekiti wa Ma Girl Guides. Mwalimu wa wengi akiwemo Profesa Tibaijuka aliyekuwa mwanafunzi wake katika shule ya Kashozi Girls Middle School Bukoba 1962-1965). Ameacha mume mtoto mmoja na wajukuu wanne.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

Taarifa ya Frank Emmanuel

Posted by on Jan 12 2018. Filed under Prof Tibaijuka's Daily Photo News. You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Both comments and pings are currently closed.

Comments are closed

Photo Gallery

Log in | This website is Designed & Maintained by Noel Mubeya