Prof  Anna Kajumulo Tibaijuka

Kumbukumbu ya Cardinal Rugambwa 12/7/1912 – 8/12/1997

Wapendwa Wanafamilia ya Mungu, Tumsifu Yesu Kristu.
Leo Ijumaa 08/12/2017 Mama Kanisa Katoliki Anafanya Sherehe ya Mama Bikira Maria Mtakatifu Mkingiwa Dhambi ya Asili, Ambapo ni Kumbukumbu ya Miaka 20 ya Kufariki Hayati Laurian Kardinali Rugambwa
Kardinali Rugambwa Alifariki 08/12/1997 Dar es salaam.

HISTORIA YA KUZALIWA, IMANI NA WITO WAKE

Hayati Laurian Kardinali Rugambwa Alizaliwa 12/07/1912 Rutabo-Kamachumu na Wazazi Wake Baba Domitian Rushubirwa na Mama Asteria Mukaboshezi
Katika Kipindi Fulani Hayati Laurian Kardinali Rugambwa Alisafiri Umbali wa Km 20 Kutoka Rutabo Hadi Parokia ya Kagondo Kufuata Mafundisho ya Katekisimu, Baada ya Kuelewa Vema Imani Katoliki Alibatizwa 21/03/1921
Hayati Laurian Kardinali Rugambwa Alichaguliwa Kujiunga na Seminari Ndogo ya Rubya 1926 na Baadaye Alijiunga na Majiundo ya Kipadre Kwenye Seminari Kuu ya Katigondo-Uganda.
Baada ya Majiundo ya Kipadre Hayati Laurian Kardinali Rugambwa Alipewa Daraja Takatifu ya Upadre 12/12/1943 na Hayati Burchard Huwiler Kwenye Parokia ya Rutabo, Vikariati ya Bukoba (Nyakati Hizo)
Baada ya Upadrisho Hayati Laurian Kardinali Rugambwa Alipangiwa Utume Wake Kwenye Parokia ya Kagondo na Baadaye Parokia ya Rubya
Hayati Laurian Kardinali Rugambwa Alitumwa Roma Kwenye Chuo Cha Kipapa Cha Urbaniana Kusomea Sheria za Kanisa (Canon Law) na Kufuzu Shahada ya Juu ya Udaktari wa Sheria za Kanisa
Hayati Laurian Kardinali Rugambwa Baada ya Masomo ya Juu ya Udaktari wa Sheria za Kanisa 1948 Alirejea Kwenye Vikariati ya Bukoba na Kuhamishiwa Kufanya Utume Wake Kwenye Parokia ya Kashozi
Hayati Laurian Kardinali Rugambwa 16/12/1951 Aliteuliwa Kuwa Askofu wa Vikariati ya Kagera Ndogo na Baadaye Alipewa Daraja Takatifu ya Uaskofu 10/02/1952 na Kukabidhiwa Jukumu la Kusimamia Parokia 5 Zilizokuwa Kwenye Vikariati ya Kagera Ndogo.
Baada ya Kupandishwa Hadhi Vikariati ya Bukoba Mwaka 1953 Iliundwa Jimbo Katoliki la Rutabo Hayati Laurian Kardinali Rugambwa Akawa Askofu wa Rutabo.
Mwaka 1960 Jimbo Katoliki la Rutabo Lilivunjwa na Kuundwa Jimbo Katoliki la Bukoba Ambapo Baba Mtakatifu Paulo XXIII Alimteua Hayati Laurian Kardinali Rugambwa Kwa Kumpa Adhama ya Ukardinali na Kumsimika Rasmi 28/03/1960
Mwaka 1969 Hayati Laurian Kardinali Rugambwa Alihamishwa Jimbo Katoliki la Bukoba na Kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam Moja ya Kazi Kubwa Alizofanya ni Kuanzisha Shirika la Masista la Dada Wadogo wa Mt.Fransisko wa Asizi la Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam, Kujenga Kituo Cha Afya Cha Parokia ya Mt.Augustino-Ukonga, Kujenga Seminari Kuu ya Mt.Karoli Lwanga-Segerea na Seminari Ndogo ya Mt.Maria-Visiga N.k
Baada ya Utumishi wa Muda Mrefu Kadri ya Sheria ya Kanisa Mwaka 1992 Hayati Laurian Kardinali Rugambwa Aling’atuka Kuongoza Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam na Kumkabidhi Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Baada ya Kung’atuka Kuongoza Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam Aliendelea Kuishi Dar es salaam Hadi Alipofariki 08/12/1997 Mwili Wake Ulizikwa Kwa Muda Kwenye Parokia ya Kwanza Kongwe ya Kashozi, Jimbo Katoliki la Bukoba na Baadaye Masalia ya Mwilima Wake yalihamishwa Kutoka Kwenye Parokia Kashozi na Kuzikwa Rasmi Kwenye Kanisa la Kiaskofu Jimbo Katoliki la Bukoba.

Kwa Upendo, Ukarimu na Utume Wake Uliotukuka Namuombea Hayati Laurian Kardinali Rugambwa Apate Pumziko la Milele Mbinguni, Amina.

Bwana alitoa zawadi kubwa sana na sisi wanufaika tunaendelea kumuombea na kumuenzi Cardinali wetu mpendwa. Kwa niaba ya wasichana wa Rugambwa girls Pioneer classes 1965/66 tuliosomeshwa bure na Cardinal hadi kumaliza kidato cha nne ninasema Baba asante. RIP Cardinal Rugambwa. Your legacy lives on. Mama T

Posted by on Dec 9 2017. Filed under Prof Tibaijuka's Daily Photo News. You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Both comments and pings are currently closed.

Comments are closed

Photo Gallery

Log in | This website is Designed & Maintained by Noel Mubeya