Matembezi ya kuchangisha fedha mkoa wa Kagera yameongozwa na Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi mjini DSM 17-09-2016
Matembezi ya kuchangisha fedha mkoa wa Kagera yameongozwa na Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi mjini DSM na kuchangisha zaidi ya Shs.Milioni mia tano.
Prof Anna Tibaijuka Mbunge wa Muleba Kusini na pia Mwenyekiti wa waBunge Mkoa wa Kagera alishiriki na kutoa neno la shukrani baada ya Mbunge wa Bukoba Manispaa Mhe Wilfred Lwakatare kuelezea matatizo yaliyokumba Mkoa wa Kagera. Matembezi yaliandaliwa na Wizara ya Mambo ya nchi za nje na kuhudhuriwa na mamia ya watu wakiwemo mabalozi kutoka nchi za nje wafanya biashara na viongozi wengine wakuu wa serikali wakiwemo mawaziri makatibu wakuu na mashirika ya umma makampuni binafsi na taasisi za kidini na kijamii.
Pichani Rais Mwinyi akiongoza matembezi akiwa na mwenyeji wake Mhe Balozi Augustine Maige Waziri wa Mambo ya Nje, Katibu Mkuu kiongozi Mhe Balozi John Kijazi na Mhe Prof Tibaijuka (Mb) kwa niaba ya watu wa Kagera.